The House of Favourite Newspapers

Kiiza nje wiki mbili

0

STRAIKA wa Simba, Hamis Kiiza atakuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili akiuguza maumivu ya nyama za paja akiwa mazoezini.

Kiiza raia wa Uganda aliyejiunga na Simab msimu huu akitokea Yanga ambaye sasa anaongoza kwa ufungaji katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao matano, alipata maumivu hayo mazoezini Jumanne iliyopita.

Wakati Mganda huyo akikaa nje ya uwanja kwa wiki mbili, kiungo mchezeshaji Mwinyi Kazimoto yeye amerejea uwanjani na kuanza mazoezi mepesi akitoka katika majeruhi ya enka.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Daktari wa Simba, Yassin Gembe, alisema uamuzi huo wa kumuweka Kiiza nje ya uwanja umekuja baada ya kumfanyia vipimo vya majeraha hayo.

Gembe alisema ndani ya wiki hizo mbili, Kiiza ataitumia wiki moja kwa kupewa matibabu na wiki nyingine ataitumia kwa kufanza mazoezi mepesi ya binafsi kabla ya kujiunga na wenzake.

Hii inamaanisha kuwa, huwezekano wa Kiiza kucheza au kutocheza mechi dhidi ya Mbeya City Oktoba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya itategemea na maendeleo ya afya yake.

“Kiiza tumemfanyia vipimo leo (jana) mchana na amegundulika ana maumivu makali ya nyama za paja yatakayomuweka nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili.

“Katika kipindi hicho chote atafanya program maalum aliyopewa na madaktari waliomfanyia vipimo ikiwemo kupata matibabu kwa wiki ya kwanza kabla ya pili kuanza mazoezi mepesi ya binafsi,” alisema Gembe.

Leave A Reply