The House of Favourite Newspapers

Kijana ateseka miaka 10, asema nakiona kifo hivihivi

0

MGONJWA SHY (3)
Mustapha Haruna akiwa amevimba tumbo na kulazwa hospitali ya rufaa Bugando, Mwanza.

Gabriel Ng’osha na Haruni Sanchawa

Eeh! Mungu tenda miujiza! Ni maneno ambayo unaweza kuyasema ukimuona Mustapha Haruna (32), mkazi wa Ndala mkoani Shinyanga anayesumbuliwa na tumbo kujaa maji baada ya moyo wake kupanuka.

CHANZO CHA UGONJWA

MGONJWA SHY (4)Akizungumza na Uwazi, kwa njia ya simu kutoka mkoani Shinyanga mama mzazi wa Mustapha,  Hidaya Mrisho alisema kuwa mwanaye alianza kuugua mwaka, 2005 baada ya kusumbuliwa na miguu, kifua pamoja na homa kali.

Akizungumza na gazeti hili Hidaya alisema:

“Nilimpeleka Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, alipopimwa alibainika kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu (TB) na kuanza kutibiwa, lakini alihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza ambapo alipimwa na kugundulika kuwa moyo umepanuka na unamwaga maji tumboni na kusababisha tumbo livimbe.

MGONJWA SHY (2)….Akiwa nyumbani kwake.

“Nimejitahidi kutumia kila namna ili kuokoa maisha  yake lakini nimeshindwa baada ya kuishiwa fedha, kwani ninatakiwa kumpeleka kliniki Bugando ila sina uwezo zaidi ya kumpeleka hospitali ya mkoa wetu.

“Mara ya mwisho nilimpeleka kliniki mwaka 2010, tangu hapo sijawahi kumpeleka kwa sababu ya kukosa fedha na kulazimika kumtibu hapa mkoani.

“Kutokana na tatizo alilonalo Mustapha, amewahi kutolewa maji machafu lita 1 mwaka 2012 alipokuwa Hospitali ya Bugando na lita 5 mwaka 2014 akiwa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

“Baadhi ya wataalam walinishauri kama nina pesa nimpeleke kijana wangu India kwa matibabu zaidi, jambo ambalo siwezi bila msaada kwa sababu kumpeleka Bugando tu, gharama zimenishinda.

MSIKIE MGONJWA

Akizungumza kwa tabu kijana Mustapha alisema:

“Kwa kweli naumwa; nakiona kifo hivihivi. Yeyote mwenye kuguswa na tatizo langu naomba anisaidie kupata matibabu, fedha za dawa, chakula na mengineyo ili niweze kurudi katika hali yangu, kwani kwa hali hii nakiona kifo kikininyemelea.

“Nawaomba Watanzania waniepushe na roho wa mauti.”

 Kwa yeyote aliyeguswa na tatizo la Mustapha anaweza kuwasiliana naye kwa namba 0764420902, 0689837790 au namba ya mama yake 0683952363 Hidaya Mrisho.

 

Leave A Reply