Kijana Jamar Bailey (21) mkazi wa Birmingham amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 25 jela mahakama ya Birmingham Crown nchini Uingereza jana Jumatatu, baada ya kujaribu kuuwa mtoto mwenye umri wa wiki tatu mwezi Juni mwaka huu.
Jamar alitumia mtandao wa Google kuuliza namna ya kuua mtoto kwa kumnywesha sumu ambapo baada ya kupima haja ndogo wataalamu wa afya waligundua kuwa alinyweshwa ‘Sodium Valporate’ dawa zinazotumika kutibu ugonjwa wa kifafa na Maradhi ya hisia (Bipolar) ambazo zinauweza wa kumuuwa mtoto mchanga.