The House of Favourite Newspapers

Kijana wa Tarime Ashinda Sh Milioni 1 ya Sokabet

Kijana wa Tarime aliyejishindia Sh milioni moja kwa kubeti kwa Sh 1,000 tu

KAMPUNI ya Sokabet imeendelea kuwaneemesha Watanzania na watu wote ambao wanashiriki katika kubashiri matokeo ambapo kijana wa Tarime amejishindia Sh milioni moja kwa kubeti kwa Sh 1,000 tu.

 

Akizungumza mara baada ya kushinda kiasi hicho, kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Chacha Marwa alisema hakutegemea kama angeweza kushinda kiasi hicho kwa kuwa alikuwa akibeti kwa kubahatisha tu.

 

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa Tarime mkoani Mara alisema kiasi hicho cha fedha kimemfikia wakati sahihi kwa kuwa amekitumia kuongeza mtaji katika biashara zake ndogondogo na kuahidi kuendelea kubeti mara kwa mara katika Sokabet.

 

“Kwa kweli sijui hata nimeshinda mechi ngapi, mimi natumia simu ya tochi, niliona tu Sokabet katika gazeti la michezo nikaamua kujaribu, nimekuwa nikifanya hivyo tangu Oktoba, mwaka jana lakini sikuwahi kushinda.

“Sasa wiki iliyopita ndipo nikabeti ile kubwa wanaiita Jackpot, usiku wa saa nne nikatumia ujumbe kuwa nimeshinda milioni moja, nikajua ni utapeli, asubuhi nilipoihamisha katika simu yangu ikakubali, nilianza kujaribu kuhamisha laki sita.

 

“Kwa kweli tangu nishinde kuna vijana wenzangu wamehamasika na wameingia katika Sokabet kwa ajili ya kubet,” alisema Chacha ambaye ana umri wa miaka 29.

 

Akizungumzia kuhusu promosheni yao ya sasa, Meneja Usimamizi wa Sokabet, Lusekelo Mwandenene alisema:

“Kuna promosheni nyingi zinaendelea na kuhusu milioni moja ya Chacha ni mwendelezo wa Jackpot ambayo inafanyika kila wikiendi ambapo mshindi anaweza kushinda hadi Sh milioni 100 kwa kubeti kwa shilingi Sh 1,000 tu.”

 

Unavyoweza kupata Sh 100m
Hapa mshiriki anatakiwa kubeti mechi 13 tu kwa shilingi 1,000 lakini kuna mechi tatu za ziada ambazo zinawekwa ili zijumuishwe katika orodha hiyo kwa dharura endapo itatokea kati ya zile 13 za awali kuna ambayo haikufanyika au haikumalizika, lakini zote zikichezwa bila tatizo, basi hazitaathiri zile 13 ambazo ndizo muhimu.

 

Ikitokea mshiriki amekosea kutabiri baadhi ya mechi bado anaweza kupata nafasi ya kujishindia mamilioni ya fedha
Mechi Fedha utakazopata
13 Sh 100,000,000
12 Sh 2,500,000
11 Sh 1,000,000
10 Sh 500,000
9 Atashiriki bure Jackpot inayofuata

Na Mwandishi Wetu

ALICHOKISEMA Masoud Djuma, Bocco Baada ya Kufanya Mazoezi

Comments are closed.