The House of Favourite Newspapers

Kijue Chakula Anachotakiwa Kula Mjamzito – Video

KIPINDI cha ujauzito ni kipindi am­bacho mama mtarajiwa anatakiwa kupata mlo ulio kamili kwa muda sahihi na kiwango kinacho­takiwa. Mlo kamili hutokana na vyakula mchanganyiko kutoka kwenye makundi yote muhimu ya vyakula. Kwenye makala yetu ya leo tunaangalia vyakula muhimu kwenye kujenga afya ya mama na mtoto anayekua tumboni.

Njia rahisi ya kupata mlo sahihi ni kupata kiwango kinachotakiwa cha chakula kutoka katika kila kundi la vyakula. Umuhimu wa lishe bora ni kuufanya mwili kuongezeka uzito, kuzuia upun­gufu wa damu, kuboresha ukuaji na maendeleo ya mtoto aliye tumboni.

Yafuatayo ni makundi tofauti ya virutubisho vya chakula ya­nayotakiwa kupewa kipaumbele kwenye mlo wa mama mjamzito.

VYAKULA VYA WANGA

Wanga (Kabohaidreti) ni chanzo kikubwa cha nishati mwilini. Vyakula vya wanga vimega­wanyika katika makundi matatu, wanga, sukari na ufumwele. Vyakula hivi hupatikana kwa wingi na kwa urahisi zaidi kwenye na­faka kama mahindi, mchele, mtama, ulezi na ngano.Vilevile, vyakula hivi hupatikana kwenye vyakula vya mizizi kama mihogo, viazi vikuu, mag­ imbi na viazi vitamu.

Vyakula hivi huusaidia mwili wa mama kutengeneza mafuta, kuupa mwili joto na nguvu. Uko­sefu wa vyakula hivi huusababisha mwili kuko­sa mafuta, kudhoofika kwa nyama za mwili na ku­pungua uzito.

VYAKULA VYA WAN­YAMA

Vyakula vinavyotokana na wanyama kama mayai au maziwa vina virutubisho muhimu sana kwa mjamzito. Mama anapata vitamini, madini na virutubisho vingi sana kutoka kwenye mazi­wa. Kwenye maziwa yanapa­tikana madini ya Calcium am­bayo husaidia ukuaji wa mifupa ya mtoto.

Vilevile kuna protini, vitamin D na phosphorus. Ieleweke kuwa mjamz­ito anahitaji pro­tini asilimia 60 zaidi ya kiwango anachohitaji mama asiye mjamzito.

JAMII YA KUNDE

Vyakula hivi ni vyanzo vya protini, ufumwele na vitamini kwa wingi. Ni vyakula ambavyo havigharimu fedha nyingi na vinapatikana kwa wingi. Maharage yana kiwango kikubwa sana cha protini ambayo hutumika mwilini moja kwa moja bila kuleta madhara.

MAFUTA

Vyakula vyenye mafuta ni kama vile alizeti, nazi, mawese, omega 3 yatokanayo na samaki na mbegu zinazotoa mafuta.

Mafuta yakiongezwa kwenye chakula hubore­sha ubora wa baadhi ya vitamini na huongeza kiasi cha nishati. Kuna baadhi ya samaki wana mafuta yenye uwepo wa virutubisho vya omega-3 ambavyo hu­saidia kuboresha ubongo, hasa wa mtoto anayekua.

Mafuta haya humsaidia bin­adamu kua na uwezo mkubwa wa kufikiria na kutunza kum­bukumbu. Pia mafuta husaidia mtoto kuzuia magonjwa kama autism, kisukari.

Pia ni kinga nzuri kwa mama kwenye kuzuia kifafa cha mimba. Mjamzito ana­takiwa kupata gramu 250 za mafuta kila siku kwa kipindi cha mwisho cha ujauzito. Hii itasaidia kujenga ubongo na mfumo wa fahamu wa mtoto aliye tumboni. Virutubisho hivi pia hupatikana kwenye mayai ya kuku wa kienyeji.

Comments are closed.