The House of Favourite Newspapers

Kikaangoni Leo, Nay: Siwezi kutulia na demu mmoja mpaka nitakapooa

0

nayKAMA kawaida ya kolamu hii kuwaletea wasanii mbalimbali wakiwemo wa muziki na filamu na kufunguka vitu vingi kuhusiana na maswali yao kutokana na maswali mbalimbali wanayoulizwa na wasomaji wetu. Wiki hii tunaye staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki `Nay wa Mitego’.

Msomaji:  Nakupo-ngeza kwa kazi zako, naomba ujibu bila kuficha kwa nini wapenzi wako wanakukimbia? 0655 626530.

Nay:  Hahaa hilo ni jambo la kawaida, nafikiri kwa sababu nikiwa na mtu naanika uhusiano na nikiachana naye pia watu wanajua labda ndiyo maana unahisi hivyo.

Msomaji: Unahitaji uwapitie mademu wangapi ili utulie na uache tabia ya kurukaruka? 0684 899791.

Nay:  Sasa hivi siwezi kulijibu hilo mpaka nikioa ndiyo nitatulia.

Msomaji: Nay kuna siku ulikuwa Oil Com Big-Brother Manzese, ulikuwa umevaa mlegezo huoni kama si sawa ukiwa kama msanii kioo cha jamii? 0713 005127.

Nay: Usinichukulie kioo cha jamii mimi ni binadamu wa kawaida tu, nimeanza kuvaa mlegezo tangu darasa la tatu kama mtu ananikubali aangalie kazi zangu si kufuatilia maisha yangu atajisumbua.

Msomaji: Bro. we ndiyo kamanda wetu wa Manzese embu niambie ukweli, mtoto ambaye Diamond anamtangaza wa kwake ni kweli wake au kauziwa basi na abiria wake sababu anamuuzisha sura balaa, naamini unajua ukweli maana wewe ni mtu wake wa karibu. 0675 927397.

Nay: Du hayo ni mambo ya kifamilia, hayanihusu siwezi kuyazungumzia kabisa.

Msomaji: Msanii gani unayemkubali Bongo? 0712 516474.

Nay: Kuna wengi ninaowakubali wakiwemo Juma Nature, Mr. Blue ambao walikuwa wananiumiza kichwa tangu kitambo hicho, pia Diamond namkubali sana.

Msomaji: Hivi jina la Nay limetokana na nini? 0714 851072.

Nay: Hilo jina nilipewa na yule demu wangu wa Kihindi akimaanisha Hapana kutokana na ugumu wa maisha niliokuwa nao.

 Msomaji: Huoni kumnyang’anya mtoto Siwema umemnyima mtoto mapenzi ya mama? 0786 875131.

Nay: Nilifanya hivyo kwa usalama wa maisha yake sababu nimemtoa sehemu hatarishi na kumleta sehemu salama ya malezi.

Msomaji: Kaka kuna nyimbo unasema kama maisha ni magumu toa kafara, huoni kama unapotosha vijana wenzio? 0714 972747.

Nay: Simpotoshi mtu, hivyo ni vitu ambavyo vipo vinatokea kwenye jamii.

Msomaji: Hivi Nay kuna kipindi nilisikia unatoka na Shamsa mara Pam D, ukweli ni upi hapo tunayepaswa kumuita shemeji? 0767 761790.

Nay: Hahaa, wote ni shemeji zenu.

Msomaji: Mimi nipo Moshi, wewe ni Mchaga wa Machame Uduru ni kweli na kama ni hivyo kwa nini huwasaidii ndugu zako wanapiga debe? 0714 300280.

Nay: Ni kweli mimi ni Mchaga wa huko na kuhusu kuwasaidia ndugu, si rahisi kubadilisha maisha ya kila ndugu sababu sina uwezo mkubwa kiasi hicho, ikifikia hatua nikawa na uwezo huo nitawasaidia.

Msomaji: Mbona muziki wako ni kawaida, tofauti na mafanikio uliyonayo nini siri ya mafanikio yako? 0657 058170.

Nay: Sidhani kama muziki wangu ni wa kawaida kiasi hicho, ila kikubwa ni mipango na malengo kama unavyojua mimi siyo mtu wa ulabu.

Msomaji: Nay nilisikia upo Team Lowassa mbona sikuoni kwenye kampeni au unahisi akianguka itakula kwako? 0683 130206.

Nay: Niliahidi nitamsapoti na kweli namsapoti kwenye mitandao na sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye kazi zangu.

Msomaji: Vipi maisha yako ya baadaye naona unabadili wasichana kama nguo, au ndiyo unakula ujana kama ulivyoimba? 0757 109690.

Nay: Mimi ni kijana na muda wenyewe wa kula ujana ndiyo huu.

Leave A Reply