Kikosi Cha Simba Chawasili Cairo, Misri – (Picha +Video)

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa leo Aprili 7, 2021 kimewasili salama nchini Misri kikitokea Dubai.

Simba ilianza safari ya kuwafuata wapinzani wao Al Ahly jana Aprili 6 kutoka Tanzania na kilipitia Dubai ambapo kilipumzika na leo kilisafiri kuelekea Misri.

Kinatarajiwa kumenyana na Al Ahly Aprili 9, Uwanja wa Taifa wa Cairo kwenye mchezo wa hatua ya makundi.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 1-0 Al Ahly na timu zote zimetinga hatua ya robo fainali.

Simba ni kinara wa kundi A akiwa na pointi 13 huku Al Ahly akiwa nafasi ya pili na pointi 8.

 

Toa comment