The House of Favourite Newspapers

KIKWETE ALIVYOTEMBELEA MAONYESHO YA SABASABA – VIDEO

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameungana na Watanzania katika maonyesho ya 43 ya  kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere kandokando ya barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 

Kikwete amefika katika maonyesho hayo leo Jumamosi Julai 6, 2019 na kutembelea mabanda mbalimbali.

Katika banda la Jeshi la Magereza lenye samani na viatu  alishauri jeshi hilo kuzalisha bidhaa zenye viwango vya kimataifa.

 

“Kazi nzuri lakini msiangalie tu viwango vya ndani mnatakiwa kufikisha viwango vya kimataifa ili na sisi tuweze kutambulika kimataifa,” amesema.

 

Kikwete pia alitembelea banda la mbegu za mazao mbalimbali, akiwa katika banda la mbegu za mahindi ameshauri wauzaji hao kutumia majina ya mbegu yenye mvuto.

 

“Mbadilishe haya majini, kama hapa naona majina ya Tumbili, Simba, Twiga wakati mwingine mkulima ataogopa kununua kutokana na haya majina,” amesema Kikwete.

 

Comments are closed.