The House of Favourite Newspapers

Kikwete amtembelea Kardinali Pengo Dubai

0
Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete amemtembelea Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo, nchini Dubai leo. Kikwete ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter leo(Ijumaa) na kueleza kuwa amemkuta Kardinali Pengo akiwa mwenye siha njema.
 

Ingawa hajaeleza amemkuta Kardinali Pengo nyumbani au Hospitali lakini askofu huyo mkuu wa jimbo la Dar es Salaam, amewahi kuripotiwa kuwa yupo nje ya nchi kwa matibabu.
“Nikiwa Dubai safarini kwenda Canada, nimemtembelea asubuhi hii Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo na nimefarijika kumkuta akiwa na siha njema.” Ameandika Kikwete.
 
Kikwete amesema amemtembelea Kardinali Pengo wakati akiwa safarini kuelekea Canada.

VIDEO: Sakata la Makinikia… Chadema Wafunguka LIVE

Leave A Reply