Kikwete Kusaidia Matibabu ya Watoto – Video

BRAZUKA Kibenki Marathoni ni mbio za nyika zitakazofanyika Septemba 15 mwaka huu ambazo zimeandaliwa na mabenki 18 yanayofanya shughuli zake hapa nchini yakiwa na shabaha ya kuchangisha fedha ili kugharamia matibabu ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo.

Hayo yamebainishwa na rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, akiongeza kuwa matibabu hayo yatafanyika katika kitengo cha Taasisi ya Moyo Muhimbili.


Loading...

Toa comment