The House of Favourite Newspapers

KILA ANAYETEMBEA NAYE… MIMBA, NIKIMWAMBIA TUACHANE, ANACHUKIA

MIMI ni mwanamke mwenye umri wa miaka 29, sijaolewa, lakini nina mchumba ambaye nilikutana naye kama miaka mitatu iliyopita, aliniambia hajaoa, nilimpenda na yeye aliniambia ananipenda.

Mwanzoni mawasiliano yalikuwa mazuri, lakini baadaye alianza kuwa bize, nikimuuliza ananiambia ni kazi, wote tunaishi Arusha, lakini ni mtu wa ahadi, inaweza kupita hata miezi hatujaonana. Akipata muda huwa tunaongea kwenye simu, lakini mara nyingi ni yeye akinitafuta.

 

Nikimwambia kuhusu kuachana anakasirika na kuniambia mimi si mvumilivu. Mwaka jana aliniambia anataka kuja kwetu kujitambulisha, niliwaambia ndugu zangu wakaandaa kila kitu, ilienda hadi siku yenyewe hakutokea, nikimpigia simu haipokelewi. Alikuja kunitafuta baada ya siku mbili akaniomba msamaha, akiniambia kuna mambo yalitokea nimsamehe.

 

Kwa kuwa nilikuwa bado ninampenda nilimsamehe, baada ya hapo ilipita kama miezi mitano hivi bila kuonana, lakini tunachati tu, mwezi huu aliniambia anataka kuja tena kwetu, ili kukwepa aibu nilimuambia mama tu, lakini huwezi kuamini tarehe ilipofika aliniambia mama yake anaumwa hivyo nisubiri, niliumia sana kwani bado ninampenda na kaniomba msamaha kweli. Anti kuna mapenzi kweli hapa?

JIBU;

Anti nakusikitikia unapoteza muda wako. Shtuka huyo ni mume wa mtu ndiyo maana anakupotezea kila mara. Jamani Anti umri wako umeenda halafu mwanaume anakupiga tarehe, unakubali tu, unatongozwa unakataa? Changamka wewe utachina ukiwa kwenu.

USHAURI WA ANTI IME | MAWASILIANO +255 684-723043

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.