The House of Favourite Newspapers

Kila la kheri Yanga, Tuichangie Serengeti Boys

0
Wachezaji wa timu ya Yanga wakifanya mazoezi.

YANGA leo ipo ugenini kucheza na MC Alger mechi ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni ya marudiano baada ya ile ya awali iliyochezwa jijini Dar es Salaam wikiendi
iliyopita.

Katika mchezo wa kwanza Yanga ilishinda bao 1-0, hivyo ili isonge mbele leo inahitaji ushindi au sare yoyote ile jambo ambalo kama wakitulia wanaweza kulifanikisha.

Yanga inapaswa kutulia na kuwaweka sawa wachezaji wake kisaikolojia ili wasitoke mchezoni kwani timu za Afrika Kaskazini zina tabia ya kuwatoa mchezoni wapinzani wao kwa hila mbalimbali.

Inatakiwa Yanga ionyeshe ukomavu wake katika michuano hii ya kimataifa ili iweze kusonga mbele na kuipeperusha vizuri bendera ya taifa la Tanzania.

Wakati tukiiombea Yanga isonge mbele, ni wakati wetu kuhakikisha tunaichangia timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys ili iweze kuwa na ushiriki mzuri katika Kombe la Mataifa ya Afrika huko Gabon.

Leave A Reply