The House of Favourite Newspapers

Kili Canvas Ndio Habari Ya Mjini Moshi Kilimanjaro

0
Meneja mpya wa Kilimanjaro Premium Lager, Irene Mutiganzi akipiga picha kwenye Kili Cnvas iliyochorwa na Msaanii wa Sanaa ya Uchoraji, Athuman Hamis(Ochu) katika Mtaa wa Kilimanjaro Avenue Manispaa ya Moshi mjini leo ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii ya kufanya mazoezi kwa ajili ya afya na kujiandaa na kilele cha mbio za Kili Marathoni zinazotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii Machi Mosi 2020 mkoani Kilimanjaro.

Kili Canvas iliyozinduliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager hivi karibuni jijini Dar es Salaam, imekuwa ndio habari ya mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa wakazi wa wageni wanaotarajia kushiriki kilele hicho.

 

Canvas hiyo yenye lengo la kuhamasisha wakimbiaji wa vitongoji mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro  na wageni kutoka Mataifa mbalimbali katika kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi Mosi, 2020 mkoani Kilimanjaro

 

Kili Canvas ni picha maalumu iliyochorwa kwa ukubwa  na msanii wa Sanaa ya Uchoraji, Athumani Hamis(Ochu) ambapo mkimbiaji yeyote akipita karibu yake anapigwa picha na picha hiyo yenye muunganisho wa teknolojia ya kisasa baadaye kumtumia picha hiyo kupitia simu yake ya mkononi. Hata hivyo mkimbiaji anatakiwa kujisajili na kupewa chip maalumu ambayo anatakiwa kuwanayo kwa maelekezo ya wataalamu hao.

 

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Primium Lager, Irene Mutiganzi alisema baada ya wakazi wa jiji la Dar es Salam kushuhudia Kili Canvas inavyofanya kazi, sasa ni zamu ya wazai wa Manispaa ya Moshi na vitongoji vyake pamoja na Wageni wote kutoka Mataifa mbalimbali kupiga picha kwenye Canvas hiyo kama kumbukumbu maalumu ya ushiriki wako wa Kili Marathoni 2020.

 

Kwa sasa Kili Canvas tumeiweka pale Keys Hoteli usikose kufika kujiandikisha kupiga picha na kuwa na kumbukumbu maalumu ya Kili Marathoni 2020.

 

Mwisho Irene aliwahimiza Watanzania tujitokeze kwa wingi mwaka huu kushiriki kilele cha mbio za Kili Marathon kama waandaaji kwani Nchi zaidi ya 52 kutoka Mataifa mbali mbali wameshadhibitisha kushiriki kwa kujiandikisha.

Leave A Reply