Kartra

Kilichojiri Hukumu Kesi ya Membe vs Musiba – Video

HUKUMU ya kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe dhidi ya mwanahabari anayejitambulisha mwanaharakati huru, Cyprian Musiba imepigwa kalenda hadi Oktoba 28, 2021.

 

Hukumu ya kesi hiyo iliyokuwa itolewe leo Jumanne Oktoba 12, 2021 na Jaji Joaquine De Mello imeahirishwa kwa sababu haijakamilika kuandikwa.

 

Wakili wa Membe, Jonathan Mndeme amesema hukumu hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 28 kwa kuwa Jaji De Mello bado hajamaliza kuiandika.

 

Katika kesi hiyo namba 220 ya mwaka 2018, Membe anamdai Musiba fidia ya jumla ya Sh10.3 bilioni kwa madai ya kumkashfu, kupitia magazeti yake ya Tanzanite.

 

Mbali na Musiba, wadaiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhariri wa Gazeti la Tanzanite linalomilikiwa na Musiba, na kampuni ya Tz Information and Media Consultant Ltd.

 


Toa comment