KESI YA MADAWA YA SHAMIM, MUMEWE ILIPOFIKIA KISUTU

KESI inayomkabiliwa blogger, Shamim Mwasha na mumewe, Abdul Nsembo,  imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na upelelezi kutokamilika. Shamim anatuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride.

 

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, amemueleza Hakimu Mkazi, Kelvin Mhina, kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika, hivyo akaomba ahirisho.

 

Baada ya kueleza hayo wakili wa utetezi, Charles Kisoka, amedai kuwa shauri hilo halina dhamana hivyo wanauonba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.

 

Wakili Wankyo ameeleza kuwa amesikia kilichozunguzwa na upande wa utetezi, hivyo akasema watawahimiza wenzao wa upelelezi wafanye haraka na tarehe ijayo wataeleza upelelezi ulipofikia.

 

Hakimu Kelvin Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi June 10, 2019, na washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu kesi yao haina dhamana.

 

Washtakiwa hao wanatuhumiwa kusafirisha dawa hizo, Mei Mosi, mwaka huu wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam,  kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.


Loading...

Toa comment