Kilichojiri Siku Moja Baada ya Kuapishwa Trump
Baadhi ya waandamanaji wakiwa na mabango barabarani.
JUMAMOSI hii mamilioni ya wanawake duniani, waliandamana kupinga kuapishwa Rais Donald Trump akiwa rais wa 45 wa Marekani. Yalifanyika maandamo makubwa mji mkuu wa Marekani, Washington.
Baadhi ya waandamanaji wakiwa na mabango barabarani.
Aidha maandamano hayo yalikulikuwa katika miji 600 tofauti duniani kote huku waandamanaji wakiwa na mabango yenye maneno na picha za kumdhihaki na kumlaaani vikali Trump.
Watu maarufu walioshiriki katika maandamano hayo ni pamoja na John Legend, America Ferrera, Whoopi Goldberg, Cynthia Nixon, Madonna, Scarlett Johansson, Jake Gyllenhaal, Emma Watson, Ashley Judd, Cher, Kristen Stewart, Charlize Theron, Katy Perry, Charlotte Church, Yoko Ono, Helen Mirren, Julia Roberts, Amy Schumer na wengine.
Inaaminika kuwa watu takriban milioni 2.2 waliandamana kutetea haki zao za binadamu.
Pamoja na miji mingi ya Marekani, miji mingine duniani iliyokndamano makubwa ni pamoja na London, Paris, Berlin, Edinburgh, Rome, Prague, Amsterdam, Stockholm, Athens, Copenhagen, New Delhi, Brussels, Mexico City, Barcelona, Manila, Toronto, Madrid, Geneva, Cardiff na Sydney.
Baadhi ya waandamanaji wakiwa na mabango barabarani.
Baadhi ya waandamanaji wakiwa na mabango barabarani.
Comments are closed.