The House of Favourite Newspapers

‘Kilichonipata Mwenzenu ni Mungu Tu’

0

Juma Rajabu akiwa na maumivu makali baada ya kuvimba mguu.

Na Makongoro Oging’

KIJANA Juma Rajabu mwenye umri wa miaka 15, mwenyeji wa Manyoni mkoani Singida yupo katika maumivu makali, kufuatia ugonjwa wa ajabu uliompata katika mguu wake, ambao anadai chimbuko lake hasa ni ajali ya kugongwa na gari iliyompata wakati akitokea dukani.

Akiwa hana wazazi wote wawili waliofariki akiwa bado na umri mdogo, Juma anasimulia jinsi alivyokutana na ajali hiyo inayomsababishia mateso kwani ili atibiwe, zinatakiwa fedha ambazo yeye binafsi hana.

“Nilikuwa nimetumwa dukani kukununua vitu, wakati narudi nyumbani ndipo likatokea gari likanigonga. Badala ya kusimama, dereva akakimbia eneo la tukio na kuniachia mzigo huu mkubwa.

“Tangu nilipopata ajali hii, sikuwahi kupata matibabu, mguu unazidi kuoza tu, nikalazimika kutoroka kutoka Singida na kuja hapa Dar, ambapo napo sina ndugu wala msaada wowote. Nilipofika sikuwa na mwenyeji, nikalazimika kufikia Posta ambako ninalala kwenye vibaraza.

“Kuna askari mmoja wa kampuni binafsi anayeitwa Titas Balili ndiye anayenisaidia, kwani hata kama nikipewa msaada wa hela kidogo ninampatia ananiwekea, huwa pia wakati mwingine ananifulia nguo zangu.

“Licha ya maumivu, mguu wangu unabadilika kila siku, nilijaribu kwenda Hospitali ya Mwananyamala, ambako waliniambia ili nitibiwe ni lazima niwe na fedha, kuna wakati nilifikiri hali hii inatokana na mguu wangu kuota tende, lakini nimeambiwa siyo tende bali ni kutokana na uchafu maana tangu nigongwe sijawahi kufanyiwa usafi wowote,” anasema kijana huyo huku akibubujikwa na machozi.

Kwa yeyote aliyeguswa na hali ya mtoto huyu na anajisikia kumsaidia, anaweza kumpa msaada wowote kupitia nambari 0788 061199 au 0713 380581, ambazo ni za askari anayemsaidia, Titasi Balili.

Leave A Reply