The House of Favourite Newspapers

KILICHOTOKEA LEO KESI YA MBOWE, MATIKO – VIDEO

KESI namba 112/2018 inayowakabili baadhi ya viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwemo Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe na wabunge wengine saba wa chama hico, imeendelea leo, Alhamisi, Februari 14, kwa kutajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

 

Kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambaye aliteuliwa kuwa Jaji, ilitajwa leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kevin Mhina, ambapo shauri la kesi hiyo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na bado linasubiri rufaa ya kupinga dhamana iliyokatwa na upande wa mashtaka dhidi ya Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, ambayo itaanza kusikilizwa Februari 18, 2019  katika Mahakama ya Rufaa.

Nyalandu ‘ALIVYOSHUHUDIA’ Mbowe Akirudishwa Segerea

 

Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 28, 2019 kwa ajili ya kutajwa huku akieleza kuwa itapangiwa hakimu mara baada ya rufaa kusikilizwa.

 

Mbowe na Matiko wanaendelea kusota rumande kutokana na kufutiwa dhamana zao  Novemba 23, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri,  ambaye kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu, kwa madai ya ya kukiuka masharti ya dhamana.

BREAKING | HALI YA MBOWE, MATIKO MAHAKAMANI LEO

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vincent Mashinji; Katibu Mkuu Bara, John Mnyika; Katibu Mkuu Zaznibar, Salum Mwalimu; Wabunge Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), Ester Bulaya (Bunda); John Heche (Tarime Vijijini) na Halima Mdee (Kawe).

 

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13 ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018 jijini Dar es Salaam.

Comments are closed.