The House of Favourite Newspapers

Kilimanjaro Lager Yapongezwa kwa Udhamini wa Mfano

0
Naibu Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Abdallah Ulega (kulia) na Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Irene Mutiganzi wakimkabidhi mfano wa cheki mshindi wa mbio za Km 42 wa wanaume Augustino Sulle wakati wa kuhitimisha mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2021 jijini Moshi mkoani Kilimanjuaro.

WADAU wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon wametoa pongezi na sifa nyingi kwa wadhamini wakuu wa mbio hizo, Kilimanjaro Premium Lager kwa kuhakikisha yanakuwa endelevu kwa miaka 19 tangu kuanzishwa kwake.

Aidha wadau mbalimbali wamesema ushahidi wa mafanikio ya udhamini wa bia ya Kilimanjaro unadhibitishwa na kuongezeka idadi ya washiriki 500 wakati yanaanzishwa hadi kufikia washiriki zaidi ya 10,000 wa sasa.

Mashindano hayo, yanatambuliwa na kuwekwa kwenye kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF), huwa linawaleta pamoja zaidi ya washiriki 10,000 kila mwaka waume kwa wake kutoka zaidi ya Mataifa 50.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Irene Mtiganzi (kulia) akizungumza kwenye hafla ya kuhitisha mbio hizo.

Akizungumzia mbio hiyo maarufu katika uwanja wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi muda mfupi baada ya kukamilika kwa mashindano ya mwaka huu, mmoja wa washiriki George Mchome alisema kuwa ameshiriki mbio hizo akikimbia zile za kilomita 21 (Tigo Half Marathon) kwa miaka 9 sasa mfululizo na kwamba katika kipindi chote hicho ameona ari ya wandaaji katika kuyafanya endelevu kila mwaka.

“Wadhamini wakuu Kilimanjaro premium lager wamefanya kazi kubwa sana katika kuboresha mbio hizi kila mwaka kiasi cha kutambuliwa na kuwekwa kwenye kalenda ya Kimataifa, kwa kweli wanastahili pongezi nyingi”, alisema mchome ambaye anashiriki kupitia klabu ya Kili Runners.

“Kilicho cha muhimu hapa ni kwamba kwa kuwa mbio hizi zinatambuliwa kimataifa, pia inatoa nafasi nzuri kwa washiriki kupata fursa ya kupata mialiko ya mashindano mengine ya kimataifa na pia kufanya vyema mpaka kupata viwango vya kushiriki mashindano ya Olimpiki”, alisema.

Washiriki wa mbio hizo wakiwa kazini.

Kwa upande wake mshiriki kutoka nchi ya Estonia, Kaarel Pehk alisema kuwa Kilimanjaro Premium Lager Marathon inatoa fursa kwa washiriki kutoka mataifa mbalimbali kuja kuyaona mazingira mazuri ya Tanzania pamoja na kuuona Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote Barani Afrika.

Akiongea kabla ya hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika, Meneja bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Irene Mutiganzi alisema kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) ina inajivunia heshima kubwa iliyopata ya kudhamini mbio kuu za kilomita 42 pamoja na zile za kiloita 5 maarufu kama Grand Malt Fun Run.

Aidha liwapongeza wandaaji, waratibu na washiriki wote wa mbio hizo kwa njia moja au nyingine kwa michango yao mbalimbali ambayo yanapelekea mbio hizo kuzidi kukua na kupata umaarufu kila mwaka.

Jamaa wakipiga mdogomdogo.

Mtiganzi pia alielezea kuvutiwa na kuridhishwa kwake na idadi kubwa ya washiriki waliojitokeza katika mbio za mwaka ambao alisema ni kutoka zaidi ya mataifa 55 duniani kote.

Alisema kupitia chapa ya Kilimanjaro premium lager wamekuwa wakifanya juhudi kubwa kwa miaka yote 19 ikiwemo kutumia usafiri wa gari moshi (treni) ili kufanya matangazo mbalimbali kupitia kauli mbio ya mbio hizo inayoitwa ‘Twenzetu Kili’.

Wadhamini wengine wa mashindano hayo maarufu Barani Afrika ni pamoja na Tigo Tanzania (21km) na Granda Malt, ambao ni wadhamini wa mbio za burudani za kilomita 5 maarufu kama Fun run.

Wadhamini wengine wakiwemo wale wa kwenye meza za maji ni pamoja na- Uniliver Tanzania, Simba Cement, TPC Sugar, Kilimanjaro International Leather Company Limited, Kibo Palace Hotel, Garda World, Keys Hotels na CMC Automobile.

Leave A Reply