The House of Favourite Newspapers

Kilimanjaro Leather Yajivunia Udhamini Kili Marathon 2021

0

Kufuatia mafanikio ya udhamini wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited (KLICKL) kinatarajia kuzalisha vifaa vya michezo ambapo kwa kuanzia kinataria kuzalisha viatu vya michezo

Hayo yameelezwa na Afisa Mahusiano na Masoko wa kampuni hiyo, Frederick Njoka wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini humo kuhusiana taasisi hiyo  ambapo alisema, uamuzi huo unalenga kuboresha michezo nchi.

“Sisi tunazalisha bidhaa aina mbalimbali za ngozi na moja wapo ya malengo yetu ya baadaye ni kuzalisha   viatu vya michezo kwa lengo la kuboresha sekta michezo nchi ni”, alisema.

Kuhusu udhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon, Njoka alisema kuwa taasisi hiyo wanajivunia kuwa sehemu ya michuno hiyo kupitia udhamini wake kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo ili ifanyiwe kazi.

“Tunajivunia kuwa sehemu ya  wadhamini wa mbio hizi maarufu; hii ni mara yetu ya kwanza tangu kuanzishwa kwake hivyo basi, tunaahidi kushirikiana na mdhamini mkuu pamoja na wadhamini katika kuhakikisha mashindano haya yanaendelea kukua”, alisema.

Aidha alisema kampuni hiyo mpya ambayo awali ilikuwa ikijulikana kama Karanga Leather Industries inazalisha bidhaa mbalimbali za ngozi vikiwemo viatu, mikanda na pochi kutokana na ngozi halisi, malighafi inayopatikana hapa nchini.

“Wito wetu ni kwa wananchi wote kuchukua hatua za kizalendo kwa kununua bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hiki ambacho kinazalisha bidhaa nzuri na zenye ubora kwa kutumia malighafi za hapa hapa nchini”, alisema.

Kiwanda cha Kilimanjaro International Leather Industries ambacho ni ubia kati ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma (PSSSF) na Jeshi la Magereza, kilizinduliwa rasmi na Rais John Magufuli Oktoba, mwaka jana.

Leave A Reply