The House of Favourite Newspapers

Kilimanjaro Premium Lager Yaasa Washiriki Marathon Wajisajili Mapema

0

Wadhamini wakuu wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon 2023 wametoa wito kwa washiriki wajisajili mapema kwani muda uliobaki ni mchache kabla ya mbio hizo maarufu ndani na nje ya nchi kufanyika Mjini Moshi.

Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli alitoa rai hiyo wakati akizungumzia maandalizi ya mbio hizo mwaka huu ikiwemo suala la usajili.

“Tunatoa wito kwa washiriki wajisajili kupitia Tigopesa kwa kubonyeza *150*01# na kufuata maelekezo au kwa kupitia www.kilimanjaromarathon.com kwani usajili bado unaendelea lakini utafungwa wakati wowote nafasi zikijaa hata kabla ya tarehe ya mwisho yaani Februari 6, 2023,” alisema na kuongeza kuwa kujisajili mapema kutawasaidia waandaaji kufanya maandalizi ya mambo muhimu mapema kama maji, ulinzi barabarani na huduma ya kwanza.

Alisema wamejiandaa na kampeni maalumu inayujulikana kama ‘tatu zetu kwa gwara yako’ ambapo  mteja anaweza kununua Kilimanjaro Premium Lager tatu zenye ujazo wa 375ml kwa Tsh 5,000.

Kilimanjaro Premium Lager imekuwa mdhamini wa mbio hizi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2003. Wadhamini wengine ni Tigo – 21km Half Marathon, Grand Malt – 5Km Fun Run. Wadhamini wa meza za maji ni TPC Sugar, Simba Cement, Kilimanjaro Water, Total Energies  wasambazaji rasmi ni GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel na CMC Automobiles.

Wakati huo huo, waandaaji wa mbio hizi wametangaza kuwa kufuatia maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Kassim Majaliwa Majaliwa, sasa mbio hizo zitajulikana kama Kilimanjaro Premium Lager International Marathon.

Waandaaji hao walisema hatua hii itasaidia kuongeza washiriki hasa kutoka nje ya nchi  na pia kuchangia katika shughuli za utalii kama vile upandaji wa Mlima Kilimanjaro, wageni kutembelea mbuga za wanyama kama Serengeti na Ngorongoro na Visiwa vya Zanzibar. Kwa sasa mbio hizi zina washiriki kutoka nchi zaidi ya 55 duniani.

Kwa mujibu wa taarifa ya waandaaji hao, mbio hizo zimekidhi viwango vyote vya mbio za kimataifa ikiwemo, kuzingatia viwango vilivyowekwa na World Athletics(Chama Cha Riadha Dunia) lakini pia na Chama Cha Riadha Tanzania, baadhi ya washindi kupimwa kwa ajili yakuzuia matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu, ruti kupimwa kitaalamu kabisa, mtambo wa kielektroniki kutumika kutunza muda, kuhusisha wataalamu mbalimbali wakati wa mbio, vinywaji vya kutosha barabarani, ulinzi wa kutosha na namba za kukimbilia kutolewa Dar es Salaam, Arusha na Moshi.

Mbio hizi, ambazo huandaliwa na Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa na Executive Solutions Limited, zitafanyika Februari 26, 2023 katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU)

Leave A Reply