testiingg
The House of Favourite Newspapers

Kilombero Sugar Wamshika Mkono Mwogeleaje Saliboko, Wampa Dola 5,000 za Kimarekani

0

Kampuni ya Sukari Kilombero (KSCL) imechangia katika safari ya elimu ya muogeleaji mahiri, Collins Saliboko kwa kutoa kiasi cha dola za Kimarekani 5,000 kama sehemu ya ada ya kozi ya Usimamizi wa Michezo katika Chuo Kikuu cha Indianapolis, Marekani.

Hafla fupi ya makabidhiano ilifanyika tarehe 25 Agosti katika ofisi za Kampuni jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Biashara, Fimbo Butallah. Katika hafla hiyo, Bwn. Butallah, alikabidhi hundi ya mfano kwa Collins Saliboko, kuashiria dhamira ya kampuni ya kumsaidia kufikia malengo yake ya elimu.

 

Uamuzi wa Kampuni kumsaidia Collins Saliboko ni mfano wa namna ambayo kampuni zinaweza kusaidia vijana wenye vipaji na kuchangia katika utengenezaji wa fursa za ajira na kujiajiri. Mchango wa KSCL katika safari ya elimu ya Collins Saliboko unathibitisha dhamira ya kampuni katika kuwekeza kwenye kuwawezesha vijana, kukuza uongozi, na kukuza ujuzi kama baadhi ya mikakati ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii kwa ujumla.

Leave A Reply