KILUWA ALIYECHEZEA SHARUBU za JPM, LUKUVI Yamkuta Ikulu – Video

 

Mfanyabiashara Mohammed Kiluwa amejikuta kwenye wakati mgumu baada Rais Dkt. John Magufuli kuamru eneo lake la hekari 1,000 alilonunua kinyume cha sheria kwa ajili ya kufanya uwekezaji wa viwanda wilayani Kibaha mkoani Pwani.

 

Hayo yamejiri leo Juni 7, 2019 wakati Magufuli akifanya mkutano na afanyabiashara Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Kaluwa alisimama na kuelezea malalamiko yake hayo huku akimuomba Rais amrejeshee eneo hilo ili aendeleze ujenzi wa viwanda zaidi ya 10 ambavyo tayari alikuwa ameshaanza.

 

“Nilinunua eneo la hekari 50 ambapo nilijenga viwanda mpaka sasa vipo vinne, ulipokuja kuzindua kiwanda changu nilikuomba unipe eneo lingine la hekari 1,000, ulinipa maelekezo nikafuata taratibu zote nikanunua eneo hilo, nilitoa Tsh bilioni 1, nikalipa kodi ya Tsh milioni 200, taratibu zote nilikamilisha nikaanza ujenzi wa viwanda, lakini juzi nimepata barua kwamba eneo hilo liko chini ya Rais hivyo sitakiwi kuendelea na ujenzi.

 

“Ninaomba Mhe Rais uniruhusu niendelee na ujenzi, nimeongea na makampuni mengi ya nje ya nchi, nakuhakikishia ndani ya miezi minne nitakuwa nimemamliza kujenga viwanda 10 au zaidi, nikishindwa nipo tayari nifukuzwe nchi.

 

Akizungumzia hilo, Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amesema;

“Jambo la Kiluwa limezungumzwa sana, Kiluwa Free Processing Zone waliomba kumiliki ardhi ya hekari 1,000, katika Halmashauri ya Kibaha, waliambiwa thamani ya ardhi kwa hekari moja ni Tsh. Mil 5.8, lakini kwenye kikao na halmashauri walitetewa sana na mkoa, ‘msipowauzia kwa milioni 1, Mhe Rais atawapa bure kama alivyofanya kwa watu wa Bagamoyo, hivyo wakawauzia kinyume ya matarajio.

 

“Kabla ya mauziano, Mwenyekiti wa halmashauri, mkurugenzi, sektretari wa mkuu wa mkoa na mtu mwingine wa uwekezaji walipelekwa China kwanza, waliporudi mambo yakabadilika na vitu vingine walikuja navyo, watu wa TAKUKURU watajua, walimuuzia kwa Tsh milioni 1 kwa hekari, wakalazimisha wapewe eneo ulilolifuta kitu ambacho ni kinyume cha taratibu. wananchi wa pale walikuwa tayari kununua lakini hawakupewa.

 

“Kwa mujibu wa taarifa za BREALA za leo kuna mtu anaitwa KAMAKA, huyu ni Mrusi, ana shea ya 6,500 kwenye hilo eneoo, Mohammed Kiluwa ana shea ya 1,500, Kiluwa Steel Group wana shea ya 2,000, hawa ni wageni  Wachina wanajiita.

 

“Kamaka alikuja ofisni kwangu anadai Tsh bilioni nne alizompa Mohammed Kiluwa kununua lile eneo na yeye kumbe alinunua kwa Tsh bilioni moja kinyume cha sheria, kutokana udanganyifu huo hawa watu hawana viwanda, wanachukua ardhi wanadanganya na kukodisha. Timu yangu ilibaini na hati hizi zimefuntwa kwa sababu upataikanaji wake ulikuwa batili.

 

Rais Magufuli akaingilia kati;

“Unajua mimi nilimshangaa huyu Kiluwa, nilikuwa simjui alipoanza kuzungumza nikajiuliza huyu shetani amempandia waopi, kwa mujibu wa sheria ya ardhi, ardhi itapewa kwa Raia wa Tanzania tu, wawekezaji ndio watapewa kupitia TIC. haiwezekani ukachukua adhi kwa bei ndogo halafu unaiuza.

 

“Nilikwenda kufungua kiwanda chake, lakini nilipoona tu nikajua, waliokuwa wakinitolea malezo ni Wachina, kwa sababu alishakula asilimia zke nikanyamaza na mimi lengo langu ni kupata viwanda tutengneza ajira. Aliniomba mashamba ambayo tumeyafuta. Kulikuwa na haja gani ya kuyafuta ahalafu tumpe yeye?

 

“Nilimuuliza eneo lako lina hekari ngapi? Akasema 50, nikaona eneo alilokuwa amejenga haizidi hekari 2 au 3, nikamwambia ukijaza hizi heka 50 watakupa lingine, lile eneo hajalijaza lakini akafanya yake pale na mkuu wa mkoa wa Pwani akatapa eneo la hekari 1,000. Anasema ana wawekezaji wanakuja, kwa nini wasije kwenye Serikali? Yeye ndiyo utatoa hati au Rais?.

 

“Nikamwambia Lukuvi futa hiyo hati, wala usihangaike mimi ndiyo nimefuta hiyo hati. Amezunguka mpaka kwa wastaafu lakini nishafuta. Hata huyu wa TIC alitaka siku moja kuingia kichwakichwa nikamtukana kwenye simu. Ukishaambiwa na waziri elewa.

 

“Walizoea mfumo wa zamani sasa hivi hakuna, tumelipa fidia Kigamboni zaidi ya Tsh bilioni 250, tukaambiwa wanakuja wawekezaji kumbe uongo ni mambo ya upumbavu hayajawahi kufanyika kwenye nchi yoyote. Ukishawapa hutakiwi kuwauliza wala kwenda kukusanya kodi pale. Unatakiwa uwalipe fidia ya kuchimba (kusawadhidha), masharti ya ajabu, tumechezewa mno, tubadilike.

 

Tujikumbushe

Desemba mwaka jana 2018, Mfanyabiashara Mohammed Kiluwa aliachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Ilala baada ya kutomkuta na hatia aktika kesi aliyodaiwa kumpa rushwa ya Dola za Marekani 40,000 (Sawa na Sh. Milioni 90) Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

 

LIVE: Anyang’anywa ARDHI Mbele ya JPM, “Si nilikutukana? sema ukweli”

Loading...

Toa comment