The House of Favourite Newspapers

Serikali ya Kim: Korea Hatuna Corona

0

SERIKALI ya Korea Kaskazini imesisitiza kuwa mpaka sasa haina mgonjwa hata mmoja mwenye homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona licha ya ugonjwa huo kusambaa duniani na kuakumba watu zaidi ya milioni moja.

 

Mkurugenzi wa idara ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko, Pak Myong Su,  alisema hakuna mtu yeyote aliyeambukizwa virusi hivyo nchini humo kutokana na kuchukuliwa hatua za mapema za kuwakagua na kuwaweka chini ya karantini watu wote wanaoingia nchini humo.

 

“Siri ya mafanikio ni tahadhari ya mapema kimyakimya bila mbwembwe.  Corona ilipoanza China tukafunga mipaka, bandari na viwanja vya ndege na kila mgeni akawekwa karantini,” alisema Pak akiliambia shirika la habari la Agence France-Presse.

 

Ugonjwa huo hadi sasa umeua watu zaidi ya 45,000 duniani.

 

Hata hivyo, wachunguzi wamesema kwamba kwa mujibu wa watu wanaokimbia kutoka Korea Kaskazini, mlipuko wa ugonjwa huo nchini humo ni mkubwa ila watawala wanaficha ukweli huo.

Leave A Reply