Kim Kardashian Aanza Masomo ya Sheria

MWANAMITINDO ambaye pia ni Mtangazaji wa Kipindi cha Keeping Up With The Kardashians, Kim Kardashian ameamua kuingia darasani na kujifunza uanasheria. Tayari mwanamitindo huyo ameshaanza masomo kwa siri na ana miezi nane hadi sasa akichukua shahada ya sheria katika Jiji la San Francisco nchini Marekani.

 

Inaelezwa kuwa, Kim ambaye ni mama wa watoto watatu, atafanya mitihani wa mwaka wa kwanza maarufu kama ‘baby bar’ na akifaulu ataendelea na masomo kwa miaka mingine mitatu.

Akizungumza na Jarida la Vogue, Kim alisema; “Nilifikiria sana kabla ya kuamua hili…lakini nikaona natakiwa niwapiganie watu katika haki.”

 

Kanye amempongeza kwa uamuzi aliochukua huku wadogo zake, Khloe na Kourtney wakimtakia maisha mema ya masomo kwani anawakumbusha baba yao, Robert Kardashian ambaye alikuwa mwanasheria maarufu aliyesaidia kesi ya mcheza soka la Marekani na Muigizaji, OJ Simpson.

LOS ANGELES, MAREKANI

Loading...

Toa comment