Kim Kardashian: Wanawake Wakaguliwe na Wanawake Gerezani

MWANAMITINDO na mtangazaji wa televisheni nchini Marekani, Kim Kardashian West , ametaka ukaguzi magerezani ufanyiwe mabadiliko ili wafungwa wa kike wakaguliwe maungoni na askari wanawake wenzao, si pamoja na wanaume kama ilivyo sasa.

Aliyasema hayo wiki hii  alipotembelea gereza la wanawake alilofungwa maisha mwanamke Alice Marie Johnson kwa kujihusisha na madawa ya kulevya ambapo alibidi kutoa ombi hilo kwa Rais Trump wa Marekani ili amsamehe mwanamke huyo.

Ombi la mabadiliko hayo alilifikisha kwa Gavana Jerry Brown aliyesema wanalifanyia kazi.

Kim akiwa  na Trump alipokwenda kumwombea msamaha Alice Marie Johnson.

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment