KIM NANA AMNASA MRITHI WA MONDI
MUUZA nyago maarufu Bongo, Lillian Kessy ‘Kim Nana’ ambaye kuna wakati aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefungukia uhusiano uliopo kati yake na Mtangazaji wa Eatv Anthony ‘T Bway’ na kusema mambo yapo kama yanavyoonekana.
Kufunguka hivyo kwa Kim Nana juu ya uhusiano wake na T Bway kumekuja baada ya siku za hivi karibuni kusambaa kwa picha mbalimbali zikiwaonesha wawili hao wakiwa kimahaba zaidi huku watu wakihoji juu ya kinachoendelea.
“Kwa picha hizi hawa watakuwa ni wapenzi maana si kwa mikao hii. Inavyoonekana Kim Nana kapata mrithi wa Mondi sasa, acha tuone picha linavyoendelea,” aliandika shabiki mmoja aliyejiita Kacm2006 kwenye Mtandao wa Instagram baada ya kuona picha hizo. Mwingine aliyejiita Isack akaandika: “Huyu Kim si alikataa kuwa hayupo katika uhusiano na T Bway? Hivi wadada wa Bongo nani kawaroga? Kama hakuna chochote kati yao, hizi picha za kimalovee vepe?”
Baada ya kuona ishu imepamba moto, mwandishi wetu alifanya jitihada za kuwatafuta wawili hao ili kuweka wazi kinachoendelea kati yao ambapo wa kwanza kupatikana alikuwa Kim Nana, akafunguka hivi: “Sasa hapo ulitaka niseme nini wakati kila kitu umeona na kinajieleza. Umeshaona video na picha kwenye snap chat yangu, sasa niongeze kitu gani? Kama ulivyoona basi ndivyo ilivyo, sioni cha kuongeza hapo.”
Kim Nana alipoulizwa kama T Bway ndiye mrithi wa Diamond, alicharuka na kuanza kutoa povu: “Ushaanza mambo yako, huyo Diamond anakujaje, kwani alikuwa nani kwangu? Tafadhali tuheshimiane.” Alipotafutwa T Bway ili kuweka wazi kama ndiyo ameamua ‘kupumzika’ kwa mtoto huyo mzuri, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa. Jitihada za kumpata zinaendelea ili kujua kama ni penzi kweli ama kuna projekti kati yao.
Stori: Shamuma Awadhi, Amani
Comments are closed.