KIM NANA HAUZI SURA BILA MILIONI MOJA

Lilian Kessy ‘Kim Nana’

MUUZA nyago matata kwenye video za wanamuziki wa Bongo Fleva, Lilian Kessy ‘Kim Nana’ amefu-nguka kuwa kwa sasa hawezi kutumika kuuza sura kwenye video ya msanii yeyote bila kulipwa shilingi milioni moja.

 

Akizu-ngumza na Gazeti la Ijumaa, Kim ambaye miezi kadhaa iliyopita alidaiwa kutoka kimapenzi na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, alisema kuwa ameona kazi hiyo hailipi hata kidogo hivyo kama mtu atamtaka awe video queen kwenye wimbo wake, lazima amlipe kiasi hicho.

 

“Kazi hiyo kwa sasa sifanyi maana hailipi, ukilipwa sana ni shilingi laki tano hivyo mimi kucheza kwenye video ya mwanamuziki, chini ya shilingi milioni moja haiwezekani,” alisema Kim.

Stori: Imelda Mtema, Dar

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment