Kim Nana Nimekufa Nimeoza Kwa Tbway

Lilian Kessy ’Kim nana’ akiwa na mapenzi wake ambaye pia ni mtangazaji wa TV, Tbway.

VIDEO vixen maarufu Bongo, Lilian Kessy ’Kim nana’ amesema kwa sasa amekufa ameoza kwa mapenzi wake ambaye pia ni mtangazaji wa TV, Tbway.

 

Akipiga stori mbili tatu na Mikito Nusunusu, Kim Nana alisema hategemei kuja kuachana na mwanaume huyo, labda mwenyewe ndiyo aje amuache.

Jambo ambalo si rahisi kwani shoo zake si za kitoto. “ Hivi nikikuambia nimekufa nimeoza kwa huyu mwanaume huwezi kuamini, nampenda jamani na sitegemei kuja kuachana naye kabisa,” alisema Kim Nana.

 

Kim Nana alishawahi kudaiwa kutoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambapo uhusiano wao uliwahi kupewa baraka na mama wa msanii huyo, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’.

MEMORISE RICHARD


Loading...

Toa comment