Kim Nana Sina Bifu Na Lynn

 

Muuza sura kwenye video za wanamuziki Bongo, Lilian Kessy ‘Kim Nana’.

LICHA ya wote kudaiwa kuonja penzi la staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na kusemekana kuwa wana bifu kali, muuza sura kwenye video za wanamuziki Bongo, Lilian Kessy ‘Kim Nana’ amefunguka kuwa yeye video queen mwenzake, Irene Hilary ‘Lynn’ ni washkaji na hawana tatizo lolote

 

Kim aliiambia Mikito Nusunusu kuwa watu wamekuwa wakizungumza mengi kuwa ana bifu na Lynn, lakini hawajawahi kuwa maadui hata siku moja na Lynn ni kama mdogo wake na hata wakikutana wanasalimiana vizuri na kuzungumza.

Irene Hilary ‘Lynn’

“Lynn ni mshkaji wangu, hatuna bifu kabisa ndiyo maana hata hivi karibuni niliposti kipande cha video nikiwa naimba wimbo wake wa Chafu kwa lengo la kumsapoti hivyo wanaosema tuna bifu imekula kwao maana siyo kweli,’’ alisema Kim.

Stori: Memorise Richard

Loading...

Toa comment