The House of Favourite Newspapers

Kanye West Aokoka, Aja Na Albamu Ya ‘Gospo’

SIKU chache baada ya mwanamitindo wa Marekani, Kim Kardashian, kuthibitisha kuwa yeye na mumewe Kanye West wameokoka, Kanye  amethibitisha tarehe rasmi ya kuachiwa albamu yake ya Gospo iliyopewa jina la ‘Jesus Is King‘.  Albamu hiyo yenye nyimbo 12 imepangwa kuachiwa SeptembA 27,2019.

Kanye ambaye anatambulika kama Yeezus alitangaza taarifa hizo kupitia website yake ambapo alisema albamu hiyo ilipaswa kuachiwa mwaka jana kwa jina la Yandhi. Kim Kardashian pia alipost picha inayoonyesha karatasi yenye ‘tracklist’ ya albamu hiyo.

Kanye anaendesha huduma za maombi kila Jumapili  nyumbani kwake huku mashabiki wakijiuliza ni lini Kanye ameanza kuwa karibu na ukristo.   West ambaye ni baba wa watoto wannne  amekuwa akiongoza huduma za kuabudu na kuwakaribisha wanamuziki wenzake wanaokuwa wakiubariki ugeni wao kwa fleva za Gospel.

Kim Kardashian alimwambia mtangazaji aliyetaka kujua kuhusu huduma ya maombi ambayo rappa huyo amekuwa akiifanya nyumbani kwake kuwa Kanye alianza harakati za kujikomboa mwenyewe kwanza, baadaye akaanza kushirikiana na marafiki pamoja na familia.

“Safari yake ya mabadiliko ilikuwa ya kushangaza sana, hatimaye tumeokoka sasa na Kristo ndiyo kitu tunachokiishi,” alisema Kim.

Comments are closed.