Kimbunga ‘Idai’ Chaua Watu 65 – Picha 12

 

WATU 65 wamekufa mashariki mwa Zimbabwe kutokana na eneo hilo kukumbwa na kimbunga kiitwacho Ida.

Kati ya watu waliopoteza maisha ni katika shule mbili ambapo tufani hiyo iliwakumbwa usiku wa manane wakiwa wamelala.

Kimbunga hicho kimesababisha uharibifu wa miundo mbinu katika jimbo la Manicaland karibu na mpaka wa Zimbabwe na Msumbiji.

 

Jitihada za uokoaji zinaendelea huku mamia ya watu wakiwa hawajulikani waliko, hali inayohofiwa kwamba huenda inaweza ongeza idadi ya waliopoteza maisha.

Rais Emmerson Mnangagwa amelazimika kusitisha ziara yake Mashariki ya Kati na kurejea nchini mwake kutokana na janga hili.

Hata hivyo,  kasi ya kimbunga hicho inapungua japo kuwa tayari kimesababisha madhara makubwa huku takribani watu 200 wakiwa hawajulikani walipo.

Familia nyingi zinasubira kupatiwa msaada baada ya nyumba zao kubomolewa na maji japokuwa uharibifu wa miundo mbinu zikiwemo barabara, unaongeza ugumu wa kuwafikia watu hao na kuwasaidia.

Raia wa Zimbabwe wameungana pamoja na kuendelea kuchanga fedha, mablanketi na chakula kwa ajili ya wahanga wa janga hilo.

Nchini Msumbiji na Malawi kimbunga hicho kimesababisha vifo vya watu 120.

Hali ya tahadhari imetangazwa nchini Zimbabwe katika maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga hicho kilichoyakumba maeneo hayo kikiwa na mwendo wa kasi wa kilomita 177 kwa saa.

“SPIKA ni MUONGO, NASSARI Juzi Kidogo WAMUUE, Hatukubali” – LIJUALIKALI

Loading...

Toa comment