The House of Favourite Newspapers

KIMENUKA MITANDAONI! DIMPOZ, KIBA WALIAMSHA DUDE

kiba na dimpoz
KIba na Dimpoz.

Mitandaoni bhana kuna mambo! Waswahili wanasema fumbo mfumbie mjinga mwerevu atalifumbua, kuanzia jana kwenye mitandao ya kijamii, kuna mafumbo yanayoendelea ambayo baadhi ya mashabiki wameshayafumbua.

CHANZO NI NINI?

Kwa mujibu wa mashabiki wa muziki wanadai kwamba chanzo kilianzia kwenye wimbo wa rapa Fid Q, unaoitwa Fresh, ambapo ndani ya wimbo huo kuna mistari aliyoimba Diamond ya kumkashifu Kiba.
“Kunifananisha na Cinderela kwangu haiwezi kuwa fresh, Simba toka mbuga ya Tandale, naona Swala wanafosi tuwe saresare, si walitaka viti, nimewapa hadi kitanda wakalale” Hiyo ndiyo mistari inayomlenga Kiba.
Baada ya kuisikia ngoma hiyo, Kiba akapita kwenye akaunti yake ya Twitter na kujibu mapigo kwa staili ya mafumbo

kiba na dimpoz

MARA DIMPOZ NAYE KAHUSISHWA

Saa chache baada ya Posti ya Kiba, upande wa pili ukajibu mashambulizi kwa kuachia audio yenye Verse 1 kwa kupitia beat ya wimbo ule ule wa Fresh, ambapo ndani yake kamhusisha Kiba na Ommy Dimpoz.

KICHAA CHAMPANDA DIMPOZ

Dimpoz baada ya kuusikia wimbo huo, akaamua kuliamsha dude, ambalo ndiyo linazizima mpaka sasa, huku mashabiki wakiwa na shauku ya kutaka kujua upande wa pili utafanya nini.

kiba na dimpoz

NA ISRI MOHAMED/GPL

Comments are closed.