Kinana Atua CCM Dodoma, Ampigia Debe JPM – Video
KATIBU Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amefika na kuhudhuria Mkutano Mkuu wa chama hicho unaofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma, leo Jumamosi, Julai 11, 2020.
Kinana amewaomba wajumbe wa mkutano huo, watakapopiga kura wampe kura zote mgombea wao bila hata moja kuharibika ili apate faraja yao na kisha waende nchi nzima kwa umoja kutafuta kura za Magufuli wabunge na madiwani.
“Niseme mawili, kwanza niwaombe wajumbe wa Mkutano Mkuu tutakapopiga kura tumpe mgombea urais wetu kura zote bila kuharibu hata moja, bila hapana ili apate faraja na nguvu ya kuongoza. Pili, ndugu wajumbe hakuna uchaguzi ulio mwepesi kama huu.
“Sina shaka mgombea wetu wa urais (Magufuli) atapata kura nyingi zaidi ya alizopata 2015, tutapata wabunge wengi na madiwani. Niseme kitu, nimeona watia nia wengi, Jimbo la Lorya watia nia wapo 60 ila atapewa mmoja, nawaomba tuzike tofauti zetu, tukiweke mbele chama kuliko mtu,” amesema .