The House of Favourite Newspapers

Kinana: Geita Iendane na Thamani ya Dhahabu ya Mkoa Huo

0
Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amemshauri Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella kuangalia namna nzuri ya kuupanga mji wa Geita uwe na muonekano mzuri na wa kisasa na si ulivyo kwa sasa.

 

Kinana amebainisha hayo leo September 4,2022 Mjini Geita wakati wa ziara yake ya siku moja inayolenga kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuangalia uhai wa Chama hicho.

Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella

Kinana amesema Geita ni mkoa mpya ambao una maeneo mengi, hivyo ni muhimu kwa viongozi kuanzia ngazi ya maafisa mipango kuangalia namna nzuri na bora ya kuupangilia ili uwe miongoni mwa miji mizuri na inayovutia hapa nchini.

 

“Geita inayo Miradi Mingi ya Ki-maendeleo ambayo inatekelezwa ikiwemo Ofisi za Serikali na Idara zake, Makazi ya Watumishi wa Umma pamoja na Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo hivyo ni muhimu kwa Mamlaka za mkoa huo kuweka mikakati ya kuhakikisha suala la mipango miji linazingatiwa ili kuupa hadhi na muonekano mzuri” amesema Kinana.

Wanachama wa CCM wakiwa katika mkutano na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania Bara Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana

Akiwa Geita Komredi Kinana amekagua Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo ambao unagharimu Bilioni 20.1, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita ambapo ujenzi wake umegharimu Shilingi Bilioni 7.75 pamoja na Uwanja wa Mpira wa Miguu unaomilikiwa na Halmashauri ya mji wa Geita.

Leave A Reply