Kinda wa Azam FC Afanya Makubwa Uturuki

MLINZI wa Kushoto wa Azam FC, Pascal Msindo, ambaye alipata nafasi ya kufanya majaribio klabu ya Antalyaspor ya Uturuki, ameibuka na kuelezea mafanikio yake.

 

Mchezaji huyo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana atazikosa mechi zilizobaki za CECAFA, Kagame Cup zinazoendelea sasa.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu Msindo amesema kuwa; “Nimeshafanya majaribio na wanasema nipo vizuri wameniongeza muda wa mwezi mmoja ili waone kama nitawafaa.

“Ilikuwa ni ndoto yangu kuiwakilisha nchi yangu kimataifa kama wanavyofanya wengine na nitajitaidi nisiwaangushe,” alisema Msindo

 

CAREEN OSCAR, Dar es Salaam701
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment