The House of Favourite Newspapers

Kingwendu azua balaa studio

0

Kingwendu (1)Kingwendu.

Mwandishi wetu
Kingwendu bana! Juzikati alitinga kwenye Studio ya Montesino Records iliyopo Buza jijini Dar kwa ajili ya kurekodi singo yake.

Basi unaambiwa alipofika studio hapo na kuwekewa biti ili afanye mazoezi kabla ya kurekodi, alianza kuleta ukomedi wake na kuimba huku akitoka nje na kurudi ndani.

Kwa bahati mbaya sana studio hiyo ipo ndani ya nyumba ya wazazi wa prodyuza aitwaye Dno Dyuzer. Sasa ‘maza hausi’ akiwa anapika akashangaa Kingwendu anatoka akiimba huku akisema; halu haluu, acha nijipe raha duniani. Ikawa full vurumai, watu kibao mtaani wakawa wanamshangaa.

Leave A Reply