The House of Favourite Newspapers

KIOJA KUKU ‘KUBAKWA’ NA WATU

ARUSHA: Wakazi wa Mtaa wa Bonny City, Kata ya Muriet jijini Arusha, wamekumbwa na hofu ya ushirikina kufuatia kuzuka kwa kioja cha madai ya kubakwa na kunajisiwa kwa kuku wao na ‘watu’ wasiojulikana, Risasi Jumamosi linakupa undani wa tukio hili.  

 

Hatua hiyo imekuja kufuatia kuku zaidi ya 10 wa eneo hilo kubakwa na baadhi yao kufa na wengine kudhoofu kutokana na hali ya kuingiliwa na viumbe wanaoaminika ni binadamu wasiojulikana.

 

Akizungumza kwa masikitiko, mmoja ya wakazi wa kata hiyo ya Muriet, Elizabeth Swai ambaye kuku wake watano wamebakwa na baadhi yao kufa, alisema katika hali isiyo ya kawaida na wakati tofauti amekuta kuku wake wenye manyoya meupe wakiwa wamedhoofu na alipowachunguza alibaini kunajisiwa.

 

“Jambo hili limenisikitisha sana kila kukicha nakuta tetea amedhoofu nikimwangalia vizuri naona kizazi chake kimetoka nje na kimekuwa kikubwa na mbegu kama za kiume zipo pembeni yake, hili jambo kwa kweli limenifanya nisitamani kula kuku tena kwa sababu sijui kama atakuwa ameambukizwa magonjwa gani,” alisema mama huyo.

 

Ameongeza kuwa, kuku wake ambao wanaishi kwenye banda lao wengi wao walikuwa wakitaga mayai lakini baada ya kufanyiwa kitendo hicho, kwa sasa wanatoa mayai yaliyolegea na kupasuka. Akizungumza huku akimwonyesha kuku aliyeonekana kunajisiwa, Elizabeth alisema kuwa ni vigumu kuamini kwamba tukio hilo linaweza kufanywa na binadamu mwenye akili timamu lakini ameshangaa kuona kuku wake wakifanyiwa tendo hilo na binadamu asiyejulikana.

‘’Huu mtaa wetu ni kama umelaaniwa matukio ya ajabuajabu hayaishi kutokea watu wanaendekeza ushirikina sana kila kukicha nikiamka nakuta kuku wangu yupo nje ya banda akiwa amezubaa na ukizingatia banda huwa nafunga na kufuli hii ni ajabu sana,” alisema Elizabeth.

 

Kwa upande wake balozi wa mtaa huo, Abraham Mbaga amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema hata kubali matukio hayo kuendelea na kwamba wapo mbioni kualika watumishi wa Mungu kwa ajili ya kuombea eneo hilo ili matukio hayo yasijirudie tena wakiamini ni jambo la kishirikina.

 

Alisema matukio ya kuku kubakwa na kunajisiwa yamekuwa yakiripotiwa kwake na kwamba hadi sasa kipindi cha wiki mbili kuku wapatao 10 kutoka familia tofauti wakiwemo kuku wa Elizabeth, wamenajisiwa.

 

“Kwa kweli jambo hili la kuku kunajisiwa katika mtaa wangu limekuwa sugu kwani kila kukicha napata taarifa za kuku kubakwa na wahusika hawajulikani, ninachofikiria kwa sasa ni kualika wachungaji waje kuombea kwa sababu ni jambo la kusikitisha sana,” alisema Mbaga.

STORI: Joseph Ngilisho, Risasi Jumamosi

Comments are closed.