Kioja! Wapenzi wa jinsia moja wapata mtoto!

 

MPENZI wa jinsia moja wa Waziri Mkuu wa Serbia, Ana Brnabic, amejifungua mtoto wa kiume.

 

Wawili hao wote ni wanawake!

 

Ripoti zinasema kuwa mama aliyejifungua na kufahamika kama Milica Djurdjic na mtoto aliyepewa jina la Igor, wote wana afya nzuri.

 

Bi Brnabic mwenye umri wa miaka 43 amekuwa ni mwanamke wa kwanza ambaye anajihusisha katika mapenzi ya jinsia moja kuwa waziri mkuu mwaka 2017 mwezi Juni.

 

Kuchaguliwa kwake kuliwashangaza wengi kwa sababu taifa hilo halitambui ndoa za watu wa jinsia moja.

 

“Ana Brnabic ni waziri mkuu wa kwanza ambaye mwenza wake amepata mtoto wakati akiwa madarakani na vilevile ni mahusiano ya kwanza ya jinsia moja duniani kote kupata mtoto,” AFP iliripoti.

 

Bi Djurdjic ambaye anafanya kazi kama daktari, alipata ujauzito kwa njia ya kupandikiza na si ya asili.

 

Katiba ya nchi hiyo imeweka wazi kuwa ndoa inayokubalika ni ya mwanaume na mwanamke na mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja hayatambuliki kitaifa.

 

Wapenzi wa jinsia moja nchini humo wamezuiwa kuasili watoto, ingawa mtu ambaye hajaoa au kuolewa anaweza kuasili mtoto.

 

Nchi hiyo ina sheria ambazo zinawabagua wapenzi wa jinsia moja hivyo kukabiliana na changamoto za kauli za chuki, kukosa haki licha ya kwamba  wanaharakati wamekuwa wakipinga ukiukwaji huo wa haki.

 

Wakosoaji wamedai kuwa Bi Brnabic hajafanya lolote katika kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja. Na hajawahi kusema kama atapenda kuhalalishwa kwa ndoa za jinsia moja nchini Serbia.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment