The House of Favourite Newspapers

Kiongozi Wa Kundi La Kigaidi La Hezbollah, Hassan Nasrallah Ameuawa

0
Kiongozi wa kundi la kigaidi la Hezbollah, Hassan Nasrallah

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limethibitisha kuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Hezbollah, Hassan Nasrallah ameuawa katika shambulio lake la IDF dhidi ya makao makuu ya kundi hilo nchini Lebanon siku ya Ijumaa.

Akizungumza baada ya kuuawa kwa Nasrallah, Mkuu wa IDF, Ltf. Herzi Halevi amesema yeyote anayetishia raia wa Israeli tutajua jinsi ya kumfikia.

Hata hivyo Maafisa wa Hezbollah hawajathibitisha kifo cha Nasrallah huku chanzo karibu na Hezbollah kikisema mawasiliano na bosi wao huyo yalipotea tangu jana jioni.

IDF ilishambulia makao makuu ya wakala wa magaidi wanaoungwa mkono na Iran kusini mwa Beirut, na kufichua kwamba walikuwa wamemlenga Nasrallah.

Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Lebanon takriban watu wengine wawili waliuawa huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.

UTANI wa RC CHALAMILA kwa MBOWE – “MAKAMANDA KUNJA NGUMI – SERIKALI HAIJAJENGA MAABARA”….

Leave A Reply