Kiongozi wa Liberia George Weah Apongezwa Baada ya Kukubali Kushindwa
Rais wa Liberia George Weah amesifiwa kwa hatua yake ya kuonyesha kukubali kushindwa na mpinzani wake katika kinyang’anyiro cha urais na viongozi wa kutoka pande za kisias ana kanda ya Afrika Magharibi
“Huu ni wakati wa neema katika kushindwa, wakati wa kuweka nchi yetu juu ya chama, na uzalendo juu ya masilahi ya kibinafsi,” nyota huyo wa zamani wa kandanda, ambaye amehudumu kama rais wa Liberia tangu 2018, alisema.
Simu ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 57 ya kumpongeza Joseph Boakai siku ya Ijumaa usiku imeiokoa nchi hiyo, ambayo ina historia ya migogoro ya kikatili ya wenyewe kwa wenyewe, kutoka wikendi ya mvutano.
Rais mteule wa Liberia, Joseph Boakai, ambaye ameshinda rais George Weah, katika duru ya pili ya urais wa Novemba 14, anasema utawala wake utaangalia kwa karibu mikataba ya uchimbaji madini ili kuhakikisha kuwa inanufaisha nchi.
Amesema kinachofuata ni kushughulikia masuala ambayo yanarudisha nyuma nchi na kutaja ufisadi na ukosefu wa huduma za msingi.
Boakai amesema eneo muhimu ambalo Waliberia hawajanufaika nalo ni sekta ya madini, licha ya kuwa na akiba kubwa ya madini katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, ikiwa ni pamoja na almasi, dhahabu, madini ya chuma na mbao.
Nimeona rasilimali zetu zikinyonywa na maisha ya watu yanabaki kuwa mabaya zaidi, Boakai alisema,na kuongeza kuwa ataangalia kwa karibu sekta hiyo.
Alipoulizwa kama hii itajumuisha kupitia upya mikataba ya uchimbaji madini, Boakai amesema mapitio yatafuatiliwa iwapo itahitajika kufanya hivyo.