testiingg
The House of Favourite Newspapers

Kiongozi wa Upinzani Visiwa vya Shelisheli Ashtakiwa kwa Uchawi, Mtanzania Ahusishwa

0
Mahakama katika Visiwa vya Shelisheli, imemsomea mashtaka ya uchawi kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, Patrick Herminie pamoja na watu wengine saba, akiwemo Mtanzania.
Herminie ambaye anatajwa kutaka kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2025 kwa tiketi ya chama kikuu cha upinzani, United Seychelles Party (USP) amekanusha madai hayo na kueleza kuwa ni mbinu ovu za kisiasa za kumchafulia jina lake na kumfanya ashindwe kugombea urais.
Polisi nchini humo, wamesema kesi hiyo inahusishwa na tukio la miili miwili ya watu iliyofukuliwa katika Makaburi ya Kisiwa cha Mahe.
Taarifa zinaeleza kuwa Herminie na wenzake, wanatuhumiwa kukutwa na vifaa vinavyodaiwa kutumika katika uchawi pamoja na vifaa vilivyoibwa kwenye matukio ya kuvamiwa kwa makanisa kadhaa nchini humo.
Inazidi kuelezwa kwamba namba ya simu ya Herminie, ilikutwa katika mawasiliano ya Whatsapp kati yake na Mtanzania aliyekamatwa mwezi Septemba kwa madai ya kukutwa na zana za kichawi.
Mahakama imeamuachia Herminie na wenzake raia wa nchini humo kwa dhamana, huku Mtanzania akiendelea kushikiliwa mpaka mwezi Novemba kesi hiyo itakaposomwa tena.
Leave A Reply