The House of Favourite Newspapers

Kipa wa Simba Aishi Manula Akoshwa na Kampeni ya Tigo ya Zigo la Euro na Hisense

0
Mshindi wa Pesa taslimu (wapili kutoka kulia) akikabidhiwa mfano wa hundi wa pesa alizojishindia na kukabidhiwa.

Dar es Salaam 6 Julai 2024: Kipa wa Simba, Aishi Manula amekoshwa na Kampeni ya Zigo la Euro na Hisense inayoendeshwa na Kampuni ya Mtandao wa Simu ya Tigo kwa kushirikiana na Kampuni ya Vifaa vya ndani vya Umeme ya Hisense na Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Pari Match.

Manula alikoshwa na kampeni hiyo kwenye ugawaji wa vifaa hivyo ambapo washindi watatu walikabidhiwa vifaa vyao pamoja mshindi mmoja alijishindia pesa taslimu ambapo kipa huyo ambaye ni balozi wa Hisense alishiriki kwenye tukio la kutoa zawadi hizo kwa washindi.

Kipa wa Simba, Aishi Manula (kushoto) akimkabidhi zawadi, Valerian Moshiro mkazi wa Mapinga Bagamoyo, Pwani ambaye ni mmoja wa washindi wa vifaa vya nyumbani vya elekroniki.

Akizungumza kwenye ugawaji wa zawadi hizo Manula alisema anashukuru kwa uwazi uliopo kwenye kuwapata washindi wa zawadi hizo ambapo jinsi ya kushiriki ni kutumia App mpya ya Tigo Pesa au kubashiri mechi mbalimbali na kampuni ya Pari Match.

Kipa huyo aliwasihi wananchi waendelee kutumia App mpya ya Tigo Pesa Super App na kubashiri mechi mbalimbali kwa kutumia kampuni ya Pari Match ili nao waingie kwenye droo ya kushinda zawadi hizo na kusisitiza kuwa kampeni hiyo bado inaendelea na zawadi ni nyingi.

Kipa wa Simba, Aishi Manula akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kushiriki kwenye tukio la kuwakabidhi zawadi washindi hao.

Zawadi hizo zilitolewa kwenye banda la Hisense lililopo Viwanja vya Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar.

Leave A Reply