Kipa Wa Zamani Wa Simba, Yanga Auwawa Kwa Kuchomwa Moto
Taarifa za kusikitisha zilizotufikia zinadai kwamba aliyewahi kuwa golikipa wa Klabu ya Simba miaka ya nyuma, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Doyi Moke, anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa moto huko Bukavu, nchini kwao Congo.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Doyi alifariki kwa kuchomwa moto, huku sababu ikisemekana kuwa alipata tatizo la afya ya akili.
Inasemekana aliondoka nyumbani kwake asubuhi huko Bukavu akienda kumwangalia mwanaye, ndipo akakutana na umauti.
Shuhuda huyo anadai kuwa katika mji wa Bukavu kuna wimbi la vibaka wanaosemekana ni wale waliotoroka gerezani.
Doyi aliunganishwa na vibaka wengine watatu ambao wote wameuawa kwa kuchomwa moto.
Shuhuda huyo pia alidai kuwa Doyi alifungwa minyororo mikononi kisha kuchomwa moto na wananchi waliochoshwa na vitendo vya uporaji unaofanywa na vibaka hao.