The House of Favourite Newspapers

Kipini cha Penny chamkera mama’ke

0

pennyStori: Imelda Mtema, Wikienda

DAR ES SALAAM: Mama mzazi wa mtangazaji wa matukio mbalimbali ya runingani Bongo, Pennieli Mungilwa ‘Penny’ (jina limehifadhiwa) amemjia juu mwanaye huyo baada ya kukerwa na kitendo chake cha kujitoboa pua na kuweka kipini hivyo kumpa masharti ya kukiondoa mara moja.

Akizungumza na Wikienda, Penny alifunguka kuwa alipoweka kipini hicho alijua kitakuwa ni kizuri na ni moja ya urembo anaoupenda lakini kwa bahati mbaya, mama’ke hakufurahishwa nacho hivyo ameamua kukiondoa na kuacha tundu lizibe.

“Sikujua kama nitamuudhi mama hivyo aliponiambia nikiondoe, sikuona sababu ya kuking’ang’ania,” alisema Penny.

Leave A Reply