The House of Favourite Newspapers

KISA AMBER RUTTY… AMBER LULU AKATAA JINA LAKE

Lulu Euggen ‘Amber Lulu’

UAMUZI mgumu! Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ amelikataa jina lake la Amber baada ya kufananishwa na mwanadada Ruth Abubakary ‘Amber Rutty’ mwenye skendo ya video chafu.

Amber Lulu aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, hata kama ni kiki, lakini ya Amber Rutty imepitiliza kwani imewadhalilisha wanawake. Alisema kinachomfanya aachane na jina la Amber ni kwa sababu linafanana na la Amber Rutty na watu wengi wanadhani ni yeye. “Wengi wanajua ni mimi na naona ameniharibia jina hivyo natafuta jina lingine. Namuachia hilo la Amber ahangaike nalo mwenyewe,” alisema Amber Lulu.

Comments are closed.