The House of Favourite Newspapers

Kisa AS Vita… Kocha Simba Ashtuka, Asitisha Mazoezi Simba

0

KATIKA kuhakikisha anapata ushindi wa nyumbani dhidi ya AS Vita, Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes, amewataka wachezaji wake wote wa kigeni waliopo kwenye majukumu ya timu za taifa kuhakikisha wanaripoti kambini Machi 30, mwaka huu.

 

Simba itavaana na AS Ijumaa hadi keshokutwa Jumatatu lengo ni kuhakikisha wanasubiri wachezaji waliopo kwenye timu za taifa ili watakapojiunga waanze program ya pamoja kwani awali walikuwa wakifanya nane tu mazoezi.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Vita Aprili 3, mwaka huu mchezo utakaopigwa saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Timu hizo zitavaana katika mchezo wa tano wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa huko Kinshasa, Congo ambao ulimalizika kwa Simba kushinda bao 1-0 ambalo lilifungwa na Mkongomani Chris Mugalu Simba wamesitisha mazoezi kwa siku jana Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu alisema kuwa tayari wamewapa taarifa wachezaji wao wote waliopo timu za taifa kuhakikisha wanaripoti Machi 30 wakati timu zote zitakapomaliza michezo ya timu za taifa.

“Tumepanga wachezaji waliopo katika timu za taifa kuripoti kambini hadi kufikia Machi 30 kwa wale wa kigeni.“Wachezaji wa kigeni wengi mechi zao zinachezwa kati ya Machi 29 na 30, mwaka huu hivyo mara baada ya michezo hiyo haraka watatakiwa kuungana na wachezaji wenzao waliopo Stars kwa ajili ya kuanza maandalizi ya AS Vita,” alisema Rweyemamu.

Stori: Wilbert Molandi na Musa Mateja

Leave A Reply