The House of Favourite Newspapers

Kisa Bongo Fleva…Agness Wa Picha Za Utupu Ashambuliwa

       Agness Mmasi

MUUZA nyago aliyejipatia umaarufu kwa kutupia picha za utupu mtandaoni, Agness Mmasi ameshambuliwa na mashabiki baada ya kujikita rasmi kwenye Muziki wa Bongo Fleva na kuachia Wimbo wa Danga unaoonekana  kukosa maadili.

 

Akipiga stori na Mikito Nusu Nusu mara baada ya kuachia ngoma hiyo ambayo imejadiliwa sana kwa sababu ya maneno makali yaliyomo kwenye mashairi yake alisema, ngoma hiyo ameiimba kwa kuanika ukweli wa kile kinachoendelea kwenye jamii.

“Nashangaa wanaonishambulia lakini ninachojua watu wengi

 

walikuwa hawaelewi nafanya kazi gani ya kunipa umaarufu, nikaona isiwe tabu bora nitimize ndoto yangu ya kuwa msanii wa muziki, sioni kama nimeimba maneno yasiyo na maadili ni vitu ambavyo vipo kwenye jamii, “alisema.

Comments are closed.