The House of Favourite Newspapers

Kisa CD ya filamu, kijana achomwa kisu, afariki dunia!

0

IMG_0682Marehemu Maulidi Shaban enzi za uhai wake.

Suzan Kayogela na Chande Abdallah INAUMA SANA! Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Maulidi Shaban (21) ameuawa kwa kuchomwa kisu na rafiki yake aliyetambulika kwa jina moja la Dotto (16) mkazi wa Kigogo jijini Dar, kisa kikiwa ni CD ya filamu aliyomkodisha. Tukio hilo lilitokea Novemba 10 majira ya saa tatu usiku eneo la Kintiku ambapo Maulidi alikuwa na kibanda cha kuuza na kukodisha CD. Chanzo chetu kilielezwa kuwa kijana huyo aliuawa kikatili baada ya kumshtakia Dotto kwa bibi yake kwa kutolipwa pesa wala kurudishiwa CD yake. IMG-20151116-WA0003

Mtuhumiwa wa mauaji hayo.

“Alipofika nyumbani kwao alimkuta bibi yake Dotto na kumwambia kila kitu na alipoondoka majira ya usiku ndipo Dotto na rafiki yake walimfuata Maulidi kibandani kwake na kumtishia kisu. Alipotaka kukimbia ndipo rafiki yake Dotto anayetajwa kwa jina la James alimpiga mtama na kuanguka hapo ndipo alipochomwa kisu. “Watu walijitokeza kumpa msaada kwa kumpeleka kituo cha polisi maana alikuwa amejeruhiwa kifuani na mkononi, hali yake ilikuwa mbaya sana na alipokimbizwa Hospitali ya Amana, walipewa rufaa kuelekea Hospitali ya Muhimbili lakini alifariki akiwa anapatiwa matibabu,” kilisema chanzo hicho. Akizungumza na mwandishi wetu, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kigogo Kati, Ibrahim Said alisema tukio hilo limewafikia na tayari kesi imefunguliwa katika Kituo cha Polisi Magomeni na upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwasaka watuhumiwa. IMG-20151116-WA0005Mwili wa marehemu ulisafirishwa kuelekea mkoani Tanga kwa mazishi. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Leave A Reply