The House of Favourite Newspapers

KISA CHIRWA, YANGA YAWAJIA JUU TFF

Msemaji wa Yanga, Dismas Ten akieleza juu ya maandalizi ya kikosi chao kabla ya mechi na Mwadui FC, kesho Jumatano.

Katibu wa Yanga, Charles Mkwasa (kulia) akizungumza na waandishi ambao hawapo pichani. 

Klabu ya Soka ya Yanga imelalamikia hatua ya Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuchelewa kutoa maamuzi ya adhabu dhidi ya mchezaji wao Obrey Chirwa raia wa Zambia.

 

Akizungumzia juu ya jambo hilo leo Jumanne, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amelalamikia hatua hiyo na kueleza kuwa inaweza kuathiri mwenendo wa timu hiyo.

 

“Hatupingi adhabu hii ya Chirwa lakini tunalalamika kwamba imechelewa kutolewa. Ilitakiwa itolewe mapema na mchezaji ajue, tunasema hivyo kwa sababu wao walikuwa kimya na sisi tungemtumia kisha baadaye wangekuja kusema ndipo masuala ya kukatana pointi yangetokea,”alisema Mkwasa.

 

Katika hatua nyingine, Msemaji wa  kikosi cha Yanga, Dismas Ten amesema kwamba kikosi chao kimekamilika kabla ya mchezo wao wa kesho Januari 17, 2018 dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga, utakaopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Comments are closed.